About

Welcome To Consoel

ABCEO – Tunatetea Uhai wa Misitu Yetu

African Blackwood Conservation & Ethnobotanical Organization imeanzishwa kwa lengo la kushughulikia changamoto za ukataji miti kupita kiasi, uharibifu wa misitu, na kupotea kwa maarifa ya jadi kuhusu mimea tiba. Tumekuwa mstari wa mbele katika kupanda na kulea miti asilia, kutoa elimu, kufanya utafiti, na kuunganisha nguvu za jamii.

Historia Yetu

ABCEO ilitokana na juhudi za waanzilishi waliotambua kuwa Mpingo una thamani isiyo na kifani katika:

  • Utengenezaji wa ala za muziki
  • Mchongoko wa vinyago
  • Tiba za jadi
  • Uhifadhi wa viumbe hai

Kwa miaka mingi Mpingo umekuwa ukikatwa kwa kiwango kikubwa bila urejeshwaji wa kutosha. Hii ilipelekea ABCEO kuanzisha miradi ya uhifadhi na ufufuaji wa spishi hii pamoja na miti mingine muhimu.

Leo, tunafanya kazi katika wilaya za:

  • Moshi Mjini
  • Moshi Vijijini
  • Mwanga
  • Arumeru
  • Hai
  • Miji na vijiji vya mkoa wa Kilimanjaro na Arusha

Dhamira Yetu

Kukuza uhifadhi wa Mpingo na miti asilia kupitia upandaji, utafiti, elimu, na ushirikiano wa jamii.

Maono Yetu

Kuona misitu ya kanda ya kaskazini ikiwa starehe, hai, na endelevu, huku jamii ikiwa na ufahamu mpana wa umuhimu wa kuhifadhi.

Malengo Yetu