Karibu

African Blackwood Conservation & Ethnobotanical Organization

Panda mti, Linda kesho

Mpingo ni urithi, tuulinde.

Kuhusu sisi

ABCEO

Karibu African Blackwood Conservation & Ethnobotanical Organization (ABCEO) ni taasisi ya mazingira inayojitolea kulinda, kurejesha na kukuza uoto wa asili hususani mti wa Mpingo (Dalbergia melanoxylon) pamoja na mimea ya dawa ya jadi. Tunafanya kazi kwa karibu na jamii, shule, makanisa, vikundi vya vijana, serikali na taasisi mbalimbali ili kuhakikisha urithi wa misitu ya kaskazini mwa Tanzania unalindwa kwa vizazi vijavyo. Mpingo ni mti wenye historia ndefu, matumizi ya kiutamaduni na thamani ya kiuchumi duniani. Kupungua kwa idadi yake kumesababisha haja ya kuongeza juhudi za upandaji, utafiti na elimu kwa wananchi. ABCEO imekuwa sehemu ya kazi hii kwa zaidi ya miongo kadhaa.

More About Us

Tunachofanya

Piga Hatua Nasi